Mfalme 👑🇹🇿
Mfalme 👑🇹🇿

@MfalmewaX

10 تغريدة 4 قراءة Feb 18, 2023
MAZOEZI BORA KWA MTU MWENYE UZITO MKUBWA ANAYEANZA MAZOEZI (OBESE)
PART 2
UZI 🧵
Sio Mazoezi ya wepesi tu, Mazoezi ya kutumia Nguvu Husaidia watu wenye Uzito Mkubwa (Obese).
Hasa kutengeneza Misuli na kuchoma mafuta kwa ufanisi Sana ...
..Kama Unataka Mazoezi ya Obese kwa Mwanaume au Mwanamke, Haya ni Mazoezi Bora ya Nyumbani ya kuzingatia?
...Shuka sasa 👇
1️⃣ Modified Push ups
Kama ni vigumu kupiga Push ups kawaida, Unaweza kujaribu kwa kuweka Mikono yako kwenye kitu kilichonyanyuka kama kiti, meza au benchi, kama Bado utaona Ngumu unaweza kutafuta sehemu ya Juu zaidi, kutumia Ukuta mpaka pale utakapojipata kwa push ups za kawaida
2️⃣ Modified Squats
Kufanya Squats kwa Uzito wa mwili inaweza kuwa ngumu kwa Mtu Mwenye Uzito Mkubwa,
Modified Squats, Tumia kiti kwa kukaa na kuinuka bila kujishika , unaweza kuendelea kwa kujaribu kupunguza urefu wa kitu mpaka pale utakapokuwa na Nguvu za kusimama Mwenyewe
3️⃣ knees lift with a Ball
Unaweza kutumia kitu chochote chenye uzito mdogo wa kushikika, au Dumbbell kufanya Zoezi hili. Sasa Shusha mpira wako mbele yako na peleka goti Moja vikutane, Rudi kwenye Nafasi uliyoanzia na Rudia kwa goti lingine. Lengo ni 3 sets of 10 reps
4️⃣ Side leg lifts
Lalia upande wa kulia , mkono wa kulia uwe chini ya kichwa chako na mkono wa Kushoto uwe kwenye Kiuno chako au sakafuni. Sasa Nyanyua Mguu wako wa Kushoto Juu kadri uwezavyo na ushishe chini Taratibu. Fanya mara 10- 15, Badilisha upande .Lengo ni 2-3 sets
5️⃣ Reverse Bridges
Lalia Mgongo magoti yako umekunja, nyanyua Magoti yako mpaka Usawa wa kichwa chako na Shuka taratibu, hakikisha Kiuno hakibaki Sakafuni,Rudia Zoezi lengo ni 3 sets ya 8-10 Reps. Bridges inaboresha misuli ya Matako na Mgongo wa Chini
6️⃣ Riding a stationary bike
Zoezi hili huboresha mwili wako kutumia oxygen na kuupa Moyo Nguvu, Hili ni Moja ya Zoezi la cardio Ambalo ni muhimu kwa wagonjwa wa Moyo, Dakika 20-30
MWISHO
Kupigana na Uzito Mkubwa sio kazi Rahisi, ila INAWEZEKANA , fanya Mazoezi kidogo kidogo na jipe Muda kwenye Hilo.
Usikate Tamaa kwa sababu hiyo sio jawabu la Matamanio Yako, Mabadiliko yanakuja taratibu, Ongezea kwa Mbio fupi au Matembezi Ukipata Muda...
Program Sahihi ya Mazoezi lazima ifatwe, Uvumilivu na Punguza Matarajio, Upe nafasi ya mwili wako kujitengeneza,
Andika ratiba yako
Matamanio unayoyataka itakuchukua Miezi kuyapata lakini utajivunia Miaka.. Fitness ni Safari ya Maisha yetu ya kila siku
Nifollow @ommyfitness

جاري تحميل الاقتراحات...