#TOTTechs
#TOTTechs

@TOTTechs

24 تغريدة 17 قراءة Sep 23, 2023
SABABU ZINAZOPELEKEA SIMU KULIPUKA.
Hivi karibuni tumeona matukio ya simu kulipuka zikiwemo simu za Oneplus Nord 2, Galaxy Note 7 na
baadhi ya simu ya nyingi zikiwemo simu kutoka kampuni ya iPhone, Oppo, Xiaomi, Vivo, n.k
Powered by #ElimikaWikiendi × @fiidzsocial
UZI MFUPI 👇
Kati ya matukio makubwa ya simu kulipuka ilikuwa ni simu za
Galaxy note 7 hii ilipelekea Samsung kuomba simu hizo zirudishwe kiwandani kwa uchunguzi zaidi.
Matukio ya simu kulipuka yanajirudia kila siku japo kuna makosa ya kiufundi makosa na mtumiaji.
#ElimikaWikiendi
SABABU KWANINI SIMU ZINALIPUKA.
1. Kasoro za utengenezaji.
Moja ya sababu au kasoro inayofanya simu zilipuke ni kutoka kwa watengezaji (kiwandani), Betri ya Lithium-ion ambayo hutumika kwenye smartphone inahitaji kujaribiwa vizuri kabla kusafirishwa.
#ElimikaWikiendi
Kama kuna hitilafu katika uundaji wa betri inaweza kusababisha betri kutofanya vizuri au kulipuka, Hii kwa kawaida hutokea wakati seli (cells) ndani ya betri zinafikia halijoto ya juu kabisa (critical temperature).
#ElimikaWikiendi
Halijoto (temperature) lisilo kawaida husababisha kitu kinaitwa "short circuit" yaani muunganiko usio mzuri kati ya sehemu mbili za mzunguko wa umeme. Ikitokea hali kama hii inaweza kusababisha simu kulipuka.
#ElimikaWikiendi
2. Hali ya betri.
Sababu nyingine inayopelekea simu kulipuka ni hali ya Betri, mara nyingi simu ikianguka inaweza kusabisha madhara au hitilafu ya Ndani kwenye betri, hii inapekelea betri kupata joto sana na huenda kusababisha kulipuka.
#ElimikaWikiendi
betri pia ikiharibika inaweza kuvimba au kutoa maji, hizi pia ni dalili mbaya zinaweza kusababisha madhara kwenye simu yako.
3. Kutumia chaja isiyo sahihi.
Hili ni kosa ambalo wengi wetu tunalifanya kila mara, kutumia chaja isiyo rasmi kwenye kifaa chako inaweza kuwa ni hatari
Chaja isiyo rasmi haiendani na ubora (specifications) za simu, mfano simu inauwezo wa kupokea umeme flani na chaja inauwezo wa kupeleka umeme kiwango kingine, hiyo inaweza kusababisha kuharibu betri na vifaa vya ndani kwenye betri, inaweza kusabisha simu kupata joto au kulipuka.
4. Overnight charging
Kuna sababu nyingi kwanini simu zinaungua, lakini moja ya sababu nyingine kubwa ni kuiacha simu ikichaji usiku kucha, hii inaweza kusababisha simu ipate joto isivyo kawaida na kupelekea short circuit na mwisho simu kulipuka.
#ElimikaWikiendi
Simu nyingi za kisasa zinakuja na maboresho au kifaa (chip) kinachozuia chaji kuingia mara tu baada ya simu kufika 100% , lakini kuna simu nyingi hazina hayo maboresho na ndiyo maana unasikia simu kulipuka usiku mtumiaji akiwa amelala na simu ikiwa kwenye chaji.
#ElimikaWikiendi
5. Processor kuzidiwa
Processor pia inaweza kuchangia simu yako kupata joto na kupelekea kulipuka, Chipset hata zile zenye uwezo mkubwa hupata joto endapo zinafanya kazi nyingi kwa wakati mmoja ikiwemo kucheza games nzito kama vile PUBG
#ElimikaWikiendi
ili kujikinga na hilo kwa sasa watengenezaji wa simu wameongeza kitu kinaitwa
thermal lock feature au thermal paste kwa ajili ya kulinda processor isipate joto, japo mara kwa mara hii inafeli Na kupelekea simu kulipuka
#ElimikaWikiendi
6. Kuiacha simu juani kwa mda mrefu.
Joto kubwa linaweza kuharibu betri ya simu. Joto kali husababisha cells ndani ya simu kuwa unstable na huweza kutoa gesi kama oxygen and carbon dioxide, gesi hizi zinaweza kusababisha betri kuvimba, kuharibu muundo wake na hatimaye kulipuka.
kwa hiyo inashauriwa kutoiacha simu kwenye gari mda mrefu au juani kwa mda mrefu.
7. Betri ya simu inapoingia maji.
Kipindi cha nyuma simu nyingi zililipuka sababu ya betri kuingia maji, lakini kwa simu za kisasa walau zinaweza kuzuia maji (water proof)
#ElimikaWikiendi
Lakini kwa zile simu ambazo siyo water proof endapo simu yako imeingia maji inashauriwa kuizima mpaka ikauke maji kabisa, kutofanya hizo inaweza kusababisha simu kulipuka pale ambapo umeme kwenye betri unapokutana na maji.
#ElimikaWikiendi
DALILI
Unaweza kuona dalili kwenye simu yako, mfano kusikia sauti ambazo si za kawaida kwenye simu yako au pengine kuhisi harufu ya kitu kinaungua au simu iwe na joto kali hasa wakati wa kuchaji basi toa simu kwenye chaji na iweke mbali sana.
#ElimikaWikiendi
Betri inapoanza kuvimba au kuona mabadiliko yoyote na mwonekano wa nje wa simu, hapo kuna tatizo kwenye vifaa vya ndani.
Unashauriwa uache kuitumia simu na uipeleke kwa fundi kwa ajili ya uchunguzi zaidi, kama ipo kwenye warranty basi fika dukani.
#ElimikaWikiendi
UNAWEZAJE KUZUIA SIMU KULIPUKA.
Japo si rahisi kuzuia simu kulipuka ila kuna njia kadhaa za kujikinga na hayo.
1: Tumia simu ikiwa na kava (Phone case)
Japo wengi wanaona kama mzigo lakini cover inasaidia sana endapo simu imedondoka kutopata madhara.
#ElimikaWikiendi
Simu ikianguka vitu vinavyoweza kuharibika haraka na kioo na betri, betri ikiharibika ndani inatengeneza gases zinazoweza kupelekea joto kali na kulipuka, cover inasaidia ku-protect betri isiharibike kwa haraka.
#ElimikaWikiendi
2. Hakikisha simu yako isipate Joto kali.
Adui mkubwa wa simu yako ni Joto kali, betri ya simu yako imetengenezwa ifanye kazi vizuri kwenye hali joto flani (32-95 degrees Fahrenheit) ikizidi hapo betri haiwezi kuwa stable.
Hivyo basi epuka yafuatayo
#ElimikaWikiendi
Usiweke simu yako juani kwa mda mrefu hasa wakati wa kuchaji, au juu ya kifaa kinachotoa joto, usiache simu kwenye gari kwa mda mrefu na kingine usiweke simu kwenye freezer kwa mda mrefu (baridi kali pia inaharibu betri)
#ElimikaWikiendi
3: Usiifunike simu wakati wa kuchaji.
Hii inaonekana kama kitu cha ajabu lakini huo ndio ukweli kwamba kuifunika simu au kuichaji na cover lake inaweza kutengeneza joto kali sana linaloweza kuleta madhara.
Pia inashauriwa usichajie simu yako kitandani.
#ElimikaWikiendi
4: Tumia chaja inayoendana na kifaa chako na jifunze namna ya kutunza betri.
Kuna vitu vingi vinaongelewa, lakini ukweli ni kwamba chaja ambayo haiendani na simu inaharibu betri ya simu, zingine huleta joto kali na kusababisha madhara.
#ElimikaWikiendi
Na pia jifunze namna bora ya kutunza betri yako ikiwemo kuchaji simu yako walau kwa 30% - 80% siyo lazima uchaji simu yako mpaka 100% au uiache simu kwenye chaji usiku kucha.
Pia angalia cable (waya) wa kuchajia usiwe umechubuka au kukatika.
#ElimikaWikiendi
MWISHO ×××

جاري تحميل الاقتراحات...