#TOTTechs
#TOTTechs

@TOTTechs

9 تغريدة 61 قراءة Jun 29, 2023
ADAPTER vs CHARGER
Adapta na chaja ni vifaa viwili vinavyotumika sana ambavyo mara nyingi hutumiwa kwa kubadilishana (unaweza kusema adapter lakini umemanisha chaja). kuna tofauti kati ya vifaa hivi viwili. Katika makala hii tutajadili tofauti kati ya adapta na chaja
Uzi mfupi
Ili uweze kuelewa kwa urahisi, Adapta ni kile kifaa unachoweza kuchomeka kwenye socket ukutani kwa ajili ya kupata umeme (source), ( kichwa cha chaja, power etc) chaja ni kifaa unachoweza kuchomeka kwenye adapta ili kuchaji betri ya kifaa chako (wengine husema cable etc)
Chaja inaweza kutumika sambamba na Adapta, chaja inachukua umeme kutoka kwenye adapta na kupeleka moja kwa moja kwenye kifaa pia chaja ina-regulate kiasi cha umeme kutoka kwenye adapta ili kuhakikisha kifaa kinapata umeme unaostahili kuepuka kuunguza kifaa.
Adapta ni kifaa kinachotumika kubadili aina moja ya umeme (type of electric signals) kwenda aina nyingine, mfano Power Adapter (Adapta ya umeme) hutumika kubadili umeme wa AC kutoka ukutani au socket kwenda DC ambao hutumika kuwasha computer na vifaa vingine vya kielektroniki
Adapta pia hutumika kubadili umeme (electric signal) kutoka connector (kiunganishi) moja kwenda nyingine, mfano USB Adapter inaweza kutumika kubadili USB Type-C connector kuwa USB Type-A connector.
Chaja, ni kifaa kinachotumika kuchaji betri au kifaa kingine kinachoweza kuchajiwa tena. Chaja inaweza kutengenezwa ndani ya kifaa unachochaji, kama vile kompyuta au smartphone, chaja inaweza kuwa kifaa tofauti ila kiwe kimeunganishwa na kifaa kinachochajiwa.
Moja ya tofauti kati ya Adapta na Chaja ni jinsi zinavyotumika, adapta inatumika kuvipa nguvu (power) au kuwasha vifaa ya kielektoniki lakini chaja hutumika kuchaji betri, adapta kawaida umeme wake unaotoka (output) haubadiliki (fixed) lakini chaja umeme hubadilika kulingana...
Na aina ya betri au uwezo wa betri/kifaa kinachochajiwa.
Adapta na chaja inaweza kuonekana kufanya kazi moja ila ziko tofauti, Adapta wakati mwingine inaweza kufanya kazi kama Chaja lakini Chaja haiwezi kukupa umeme sawa na Adapta.
Mfano kama Laptop imekufa Battery maana yake chaja haiwezi kuchaji battery badala yake unatumia Adapter kuwasha au kuipa umeme computer moja kwa moja.
Hiyo ndiyo maana halisi kwamba adapter inaweza kutumika kama chaja lakini chaja haiwezi kutumika kama adapter.

جاري تحميل الاقتراحات...