Mfalme 👑🇹🇿
Mfalme 👑🇹🇿

@MfalmewaX

18 تغريدة 51 قراءة May 16, 2023
KUNA SOMO KUBWA HAPA MFALME!
•Uchumi unashuka
•Kodi zinapanda
•Kama kipato chako ni chini ya Laki 4
👉Usichanganyikiwe
Soma huu uzi 🧵by @amerix
1.Ishi nyumba yenye thamani ya 30% ya Mshahara wako
•Usiishi kwa ndugu au wazazi
•Lipa kodi
•Maumivu ya kulipa kodi yatakufundisha kujitegemea, nidhamu & kufanya kazi Kwa bidii.
2. Akiba
•Weka Akiba 20% ya mshahara wako.
•Weka Akiba na SACCO.
•SACCOs ni rafiki Kwa hela zako.
•Ndani ya Miezi 6, Utapata mkopo nafuu wa kuwekeza au kuendelea biashara zako.
NB: Huhitaji mdhamini, Akiba yako itakushamini.
3. Bajeti
Bajeti hivi:
- Chakula
- Usafiri
- Umeme & Maji
- Urembo
Weka nidhamu kubajeti haya.
Nitakwambia kivipi.
3/a. Chakula
•Kula mara moja kwa siku au mara mbili kwa Siku( 2MAD- Two meal a Day)
•Epuka chai ya asubuhi, haina maana. Huhitaji Hilo.
•Waombe wazazi wako wakutumie chakula kijijini au nenda sokoni Jumamosi mapema utapata vyakula vizuri vya Shamba.
•Usile hotelini.
•Pika chakula chako nyumbani
•kama unatakiwa kula 2MAD, pika chakula na beba kwenye chombo.
•Epuka sukari, soda, mkate, juisi, maziwa ya kiwandani, yoghurt. Ni matakataka.
•Tumia mafuta ya wanyama kupikia
Nyanya za dukani ni gharama na hazina maana. zipotezee.
3/b. Usafiri
•Ishi karibu na kazini
•Tembea unavyoenda kazini kama haina ulazima wa Kuwahi.
•Tembea kurudi nyumbani
•Hela utakayoiweka kwa kutembea itakusaidia kununua baiskeli.
•Usiombe lift
4. Umeme & Maji
•Usikae ndani muda wote. Tunza umeme.
•Tv, redio & Sabufa sio lazima. Huvihitaji. Usinunue kwa sababu wengine wamenunua.
•Hifanyi maji kwenye madumu. Itakusaidia maji yakikatika.
5. Simu & Mitandaoni
•Tumia bando lililopunguza au yenye gharama nafuu.
•Epuka kukopa salio
•Usimiliki simu kwa mkopo (promotion)
•Zima background data & jitoe huduma za subscriptions.
•Tumia WiFi ya kampuni au kazini.
6. Usafi & Urembo
Nunua vifuatavyo
•2 vipande vya sabuni
•Mafuta mgando
•Tumia chumvi & Sodium bicarbonate (baking soda) kupiga mswaki
•Kiwi & brashi
•Hydrogen peroxide ni nzuri kuua vijidudu & sanitizer
7. Jifunze ujuzi
-Siku moja ya weekend, jiunge:
• Sehemu za ujenzi
• Gereji
• Wanapotengeneza samani
Waombe kuwa unataka ujifunze wanavyofanya.
Kuwa mpole & jifunze, Usitarajie kulipwa.
8. Anza kuuza kitu kuongeza kipato chako:
•Angalia uuze nini. Ingia makubaliano awe dalali.
•Ingia mlango kwa mlango uza mfano Soksi, Tai, mikanda
•Ingia geti kwa geti, omba kusafisha magari, ofisi, makapeti.
9. Mtandao
•Mtandao wako ndio utajiri wako.
•Jiunge gym au michezo & mazoezi mfano jogging, chandimu & kikapu.
•Utakutana na watu watakaokupa nafasi & michongo.
Kama mwili & afya ya akili inavyokuwa na Mtandao wako utakuwa pia.
10. Ishi peke yako
•Usijihusishe na wanawake, watakupoteza.
•Usinywe pombe.
•Epuka kubeti, kamali na kuwekeza hela mtandaoni. Utapoteza pesa zako.
•Usipige punyeto au Kuangalia porno, zitashusha kujiamini & hali ya kupambana.
Bonasi:
Usilinganishe kurasa yako ya kwanza na kurasa ya 12 ya mwingine.
Maisha ni safari.
Furahia kila sehemu yake.
Muhimu: Jitambue & zingatia malengo yako.
Wewe ni MFALME.
Jivunie kuwa wewe
Pambana>ushibe>uzalishe
Kuna Siku mbaya na siku nzuri kazini. Chukua somo siku zote.
Kaa mbali na wanasiasa, hao ni kenge tu.
Pambana kuwa bora zaidi ya Jana.
Ishi maisha ya kumpendeza Mungu.
SUMMARY;
1. Ishi Nyumba yenye thamani ya 30% ya kipato chako
2. Weka Akiba
3. Panga bajeti
4. Umeme & Maji
5. Simu & Mitandaoni
6. Usafi & Urembo
7. Jifunze ujuzi
8. Anza kuuza kitu Kuongeza kipato chako
9. Mtandao
10. Ishi peke yako
Kama umejifunza kitu kipya , Retweet iwafikie na wengine.
NB: Unfollow page zisizokuingia kitu kichwani, jisogeze karibu na watu wenye malengo
Follow @ommyfitness Turn on notifications post
Kwa video za Mazoezi, program za Mazoezi, Afya ya Uzazi , KARIBU DM

جاري تحميل الاقتراحات...