#TOTTechs
#TOTTechs

@TOTTechs

8 تغريدة 36 قراءة May 09, 2023
Kuna mtu alituma ujumbe DM anataka tumsaidie kuchagua processor nzuri kati ya hizi.
Intel Core i5-8600K na Intel Core i7-8700K
Kwa niaba ya wengi, tunaweka ufafanuzi hapa.
Kwanza hizo processor mbili ni Intel's 8th generation Coffee Lake series lakini ziko tofauti 👇
1: Core Count na Hyper-Threading
Core i5-8600K iko na 6 cores na 6 threads, lakini Core i7-8700K ina 6 cores na 12 threads...hivyo Core i7-8700K ina Hyper-Threading technology na inaweza kuhudumia tasks/kazi nyingi kwa wakati mmoja na nzuri kwenye multithreaded applications
2: Base speed na Turbo Clock Speed.
Tukianza na Core i5-8600K ina base clock speed ya 3.6 GHz (hii ni speed yake original) na inaweza kufanya turbo boost mpaka 4.3 GHz (tunaita ku-boost processor/kuongeza speed)
Lakini upande wa Core i7-8700K ina base clock speed ya 3.7 GHz na inaweza kwenda turbo boost mpaka 4.7 GHz. Hii inamaana kwamba i7-8700K ina high clock speed, inaweza ku-translate au kuchakata taarifa kwa haraka zaidi kwenye ulizo au kazi flani (single-threaded applications)
3: Cache:
Zote processors zina 9MB of cache, lakini i7-8700K ina faster cache kutokana na clock speed yake kuwa kubwa, cache ni taarifa zinazotunzwa kwa mda mfupi au pindi utumiapo huduma flani, mfano umefungua program kama hujaizima always inakuwa nyepesi ukufungua tena.
Gharama: Core i7-8700K ina gharama kubwa kuzidi Core i5-8600K na inawekwa kwenye kundi higher-end processor with more advanced features.
Overall:
Core i7-8700K ina-offer better performance hasa kwa multithreaded applications, Nafikiri wengi mnashindwa kuelewa hizi Multithreaded Apps/programs hizi ni programs zinazowasiliana na Processor mara nyingi zaidi endapo unafanya kazi, mfano ukiwa unatype kwenye
Microsoft Word, kuna threads zizatumika kufanya Spelling na Grammer checks, display document, check capital letters etc kwa wakati mmoja.
Core i5-8600K ni nzuri tu maana ina turbo boost speed kubwa.
All in all choice inategemea na matumizi na bajeti.

جاري تحميل الاقتراحات...