#TOTTechs
#TOTTechs

@TOTTechs

4 تغريدة 9 قراءة Apr 15, 2023
Kuna mtu aliuliza swali DM akajibiwa, ni vizuri kushare ili wote tupate maarifa.
Swali: Je processor ya Intel Core i7 6700 (6th generation) ni nzuri kwa gaming?
Jibu: Hiyo aina ya Processor ni nzuri kwa gaming, sababu zifuatazo kwanza ni 4 cores (Multi core processor)
Pia ina 8 threads, sababu ina support Intel Hyper-Threading technology kwa maana yake kila core ina 2 threads na kuifanya processor kuwa na 8 threads.
Pia base clock speed yake ni 3.4GHz na maximum turbo frequency ni 4.0 GHz, hivyo inaruhusu multitasking na kazi nzito
Hata hivyo hiyo siyo latest processor sokoni ila inaweza kusupport games za kisasa katika Frame rates nzuri, japo performance/uwezo wake kufanya kazi utategemea na vitu kama RAM, Graphics card na game husika.
Unaweza kuangalia computer yako kujua number of cores & threads
Kuangalia Number of cores kwenye computer yako. Kuna njia kadhaa
Tumia Task Manager, ukifungua Task Manager > Performance utaona cores, Logical Processors (hizi ni number of threads), processor speed, graphic etc
Pia unaweza kutumia System Information au command Line

جاري تحميل الاقتراحات...