#TOTTechs
#TOTTechs

@TOTTechs

6 تغريدة 8 قراءة Mar 18, 2023
@airtel_tanzania wamezindua huduma ya eSIM yaani haina haja ya kuweka laini ya simu, ni kitu kizuri lakini si kila simu inauwezo wa ku-support eSim.
Kwa iPhone inategemea na version ya sehemu husika, kwa US version kuanzia iPhone XR nakuendelea, Chinese Mainland hazina eSIM 👇
Kwa Hong Kong na Macao version isipokuwa iPhone 13 mini, iPhone 12 mini, iPhone SE 2020, na iPhone XS zingine hazisupport eSIM.
Samsung kuanzia S20 na Note 20 nakuendelea mpaka Z Fold/Flip 4, ila S20/S21 FE Series hazina eSIM
Google Pixel ni kuanzia Pixel 2XL mpaka Pixel 7Pro
Lakini Pixel 3 zilizonunuliwa Australia, Taiwan au Japan na zile zile Pixel 3 zenye carriers za US au CANADA (Verizon etc) hazina eSIM
Huawei ni kuanzia P40 na Mate 40 lakini P40 Pro+ and P50 Pro hazina eSIM
Oppo kuna Oppo Find X3 Pro, X5, X5 Pro, Reno 6Pro, Flip N2, Reno 5A
Lakini pia kuna simu kama Xiaomi 12T Pro, Honor Magic 4 Pro, Sony Xperia 5 IV, Motorola Razr 5G. Nokia G60, Nokia X30 na zingine nyingi, Sony ana eSIM hasa kwa latest Flagships.
Lakini pia inabidi ujue Number of eSIM supported kwenye device husika, hapa Apple anashika usukani
iPhones kuanzia 11 zinauwezo wa ku-support mpaka 20 number of eSIM, lakini kwa simu zingine ni only one (1) eSIM supported.
NAMNA YA KUJUA KAMA SIMU YAKO INAUWEZO WA eSIM
Kwa Android bofya *#06# kama simu yako inauwezo wa eSIM utaona eSIM unique identification number (EID)
Kwa watumiaji wa iPhone
Nenda kwenye Settings> General> About
Nenda kwenye “Carrier lock” utaona inaonyesha NO SIM restrictions”
Shuka chini kwenye sehemu ya “AVAILABLE SIM” halafu angalia Digital SIM au eSIM
Kuna simu ambazo ni carrier locked yaani hazi-support eSIM.

جاري تحميل الاقتراحات...