Mfalme 👑🇹🇿
Mfalme 👑🇹🇿

@MfalmewaX

10 تغريدة 19 قراءة Jan 14, 2023
DAKIKA 5 ZA MAZOEZI HAYA NI SAWA NA KUKIMBIA Dk 45
UZI 🧵
Wengi hatufanyi Mazoezi kwa sababu ya Muda
Lakini unatakiwa Mazoezi Kufanya Mara 4 kwa wiki
Tafiti zinasema kutofanya Mazoezi kuna sababisha vifo vingi sawa na Uvutaji wa Sigara na Bangi...
..Mazoezi haya Utafanya Ndani (Indoor workouts) unahitaji nafasi ndogo
Unahitaji Dakika 5 Bora kuwa fit kila siku..
Tuangalie Zoezi Moja Hadi la Tano..👇
1️⃣Side Step Shuffle (60 sec)
Ni Zoezi linalohusisha sehemu kubwa ya Mwili wa Chini Kuanzia kiunoni mpaka Miguu
Wakati wa kufanya Zoezi hili, zingatia Kuongeza speed Maana ni Rahisi, Jipe changamoto
Video imeonesha nimeswing mara 1 ila inatakiwa mara 2, Kushoto 1,2 na kulia pia
2️⃣ Mountain climbers (60 sec)
Zoezi linahusisha tumbo, stamina ya core, Mikono Sana Sana Mabega
Ni Rahisi kufanya lakini Jipe changamoto kwa kupeleka Miguu kwa haraka kidogo kwa Matokeo ya Haraka Zaidi
Linaondoka kitambi na kushusha kiwango cha Mafuta mwilini
3️⃣ Flutter kick (60 sec)
Unaweza ukalala kabisa sio lazima uinuke kama inavyoonesha video
Halafu Miguu yako unainyanyua kidogo Nyuzi 30 unaanza kupishanisha
Inasaidia kujenga Misuli ya tumbo, kitambi na stamina ya core
Ni gumu kidogo so pumzika na endelea Tena mpk ukijipata
4️⃣ Jumping jacks ( 60 second)
Nilishawahi kulielezea Zoezi hili na Faida zake na @swadakta_ alikazia pia umuhimu wake hasa kwa wanaume
Linahusisha sehemu zote za Mwili, pia ku-restore Nguvu za kiume
Hauhitaji kwenda Gym Wala uwanjani Kujaribu Hii
5️⃣ Simple High knees (60 second)
Ina imarisha Misuli ya Mapaja na Miguu, Misuli ya Mapaja ya Ndani, Ina sapoti kufunguka kwa Hips, uwezo wa Misuli kufanya kazi, balance
Ukilifanya kwa speed zaidi, inaweza Kuimarisha nguvu ya Mwili wa Chini
..Sio Lazima uwe na Uwezo kumaliza Ndani ya Dakika Moja, Hapana.
Unaweza kufanya utakapochoka , unapumzika na kuendelea, Lengo ni Dk 1 kuisha
Yakiingia kwenye mwili utazoea na kuhisi unahitaji changamoto Mpya, Wakat huo umeshaona faida ya mazoezi itakupa moyo wa kuendelea...
NASHAURI UWE NA STOP WATCH, SIMU NI DISTRACTION
Kindly Retweet, Like Comment
Nifollow @ommyfitness kwa Tips zingine zaidi
Ukiwa na Swali Niulize DM au Uzi Gani mwingine nilete
#fitness #healthylifestyle #exercise

جاري تحميل الاقتراحات...