#TOTTechs
#TOTTechs

@TOTTechs

10 تغريدة 1 قراءة Apr 10, 2023
Kwanini CEOs na Co-Founders huchukua mshahara wa $1?
Kuanzia kwa Elon Musk, Larry Page, Mark Zuckerberg, Bill Gates mpaka kwa Steve Jobs na wengi wengi, kwanini hawa rich CEOs na waanzilishi wa kampuni kuchukua mshahara wa $1?
Nini kipo nyuma ya pazia?
Uzi mfupi 👇
1. Kweli, sababu ya msingi na dhahiri ni kodi
Waanzilishi-wenza (Co-Founders) na Wakurugenzi Wakuu (CEOs) wengi huchukua mishahara ya chini, kama $1, ili kuepuka kulipa ushuru wa mapato ya juu ( High income Tax) ambao ungetozwa kama watachukua mamilioni ya dola katika mshahara.
Je, unajua kwamba mapato ya kila mwaka ya zaidi ya dola nusu milioni ($500K annual income) hutozwa ushuru kwa zaidi ya 37% nchini Marekani?
Nchini India pia, mtu yeyote anayepata zaidi ya 50 Lakh kwa mwaka, hutozwa ushuru kwa 42% ya mapato!
2. Stock Compensations (Malipo ya Hisa)
Badala ya malipo makubwa, Wakurugenzi wakuu na waanzilishi wenza huchukua hisa za kampuni kama Faida (equity of the company as compensation)
kwa nini?
1) Kodi ya faida inayopatikana kutokana na mauzo ya hisa ni ya chini sana kuliko kodi ya mapato.
2) Faida ya mtaji hutozwa ushuru tu pindi unapouza hisa (Capital gains are taxed only when you sell the equity)
Ndiyo maana hawataki mshahara mkubwa wanataka Hisa
3. Kujiamini kwa Mwekezaji
Hawa matajiri wanapopokea fidia ya hisa, utajiri wao unahusishwa moja kwa moja na utendaji wa kampuni, kwahiyo kampuni itaonekana inafanya vizuri zaidi.
(As these CEOs receive stock compensation,their wealth gets tied to the performance of the company
Hii inaleta hali ya kujiamini kwa wawekezaji.
Kadiri kampuni inavyofanya vizuri ndivyo hisa zitakavyopanda na ndivyo Mkurugenzi (CEO au Co-Founder) atakavyokuwa tajiri zaidi!
(The better the company performs, the higher the shares will rise and the wealthier the CEO will get!)
4. Maisha ya kifahari
Haya yote ni sawa, lakini hawa jamaa, wanaishi vipi maisha yao ya kifahari kwa mshahara wa $1?
Wakurugenzi wakuu wanaoendesha makampuni makubwa hupokea marupurupu mengi kuanzia likizo, huduma ya usafiri, makazi mazuri, elimu ya watoto na mengi zaidi!
5. Mkopo
Sasa Wakurugenzi Wakuu hawa huchukua mikopo kwa kiwango cha chini kabisa cha riba kwa kuweka fidia yao ya hisa kama dhamana.
Tumeona huko nyuma kwamba hawachukui mshahara bali huchukua hisa kama Faida ambayo itawalinda kwenye mikopo kuliko Salary
6. Kurejesha(kulipa) Mkopo
Mikopo iliyochukuliwa inaweza kulipwa kwa urahisi kwa kutumia gawio lililopokelewa, kutoka kwa hisa za kampuni wanazoshikilia, yaani unachukua mkopo kwa riba nafuu ukilindwa na hisa zako, hisa zako hizo hizo zikizalisha ndiyo zinalipa mkopo.
END.

جاري تحميل الاقتراحات...