Swed Junior
Swed Junior

@Kingvannytz_

11 تغريدة 54 قراءة Dec 22, 2024
STORY YA KUSISIMUA YA BINTI ALIYEKUWA AKINYONYWA DAMU YA HEDHI NA MCHUMBA WAKE TAJIRI.
Sehemu Ya Kwanza
Nb: Usichukulie Serious 😃
Open Thread 🧵...✍️ x.com
HUYU BINTI BADO YUPO KWENYE MAOMBI YA KUFUNGULIWA KUTOKA KWENYE VIFUNGO MBALIMBALI USHUHUDA WA KWELI KUTOKA KANISANI
ANAANZA KWA KUSIMULIA
Pastor Anni Mimi ni Binti mrembo na msomi, Mimi ni Mtu mwenye kibali sana. Popote nitakapoenda au nitakaa huwa watu wanafurahiwa na uwepo wangu na wengi huwa wanatamani nisiondoke. Kazini kwangu nimekuwa ni Mtu ninaependwa sana na Boss wangu kutokana na ufanyaji kazi wangu. Wazazi wangu wameokoka na ni watu wa kusali sana ila Mimi sijasimama kivile kama wazazi, japo naenda Ibadani nasali ila sometimes nimekuwa nikianguka anguka.
Nimekuwa na mahusiano na vijana kadhaa na nimeachana nao sio kwasababu ya chochote ila ni kwasababu ya maono niliyonayo. Kwa umri wangu huu sihitaji kijana mdogo nataka kijana mkubwa aliyekomaa tufunge Ndoa tujenge familia. Sikutaka tena mambo ya u Boyfriend na kuchezeana.
Pastor ninafanya kazi kwenye kampuni na maranyingi sana huwa nashinda bandarini kwaajili ya kusimamia kazi.
Siku moja nikiwa pale bandarini alitokea Mkaka mkubwa smart sana, ananukia balaa. Kwa muonekano tu alionyesha kuwa ni tajiri sana. Akanisalimia akaniuliza unafanya nini kila siku nakuona huku nikamwambia niko kazini, akasema hata Mimi nina nina fanya biashara na niko kusimamia mizigo yangu. Akaniomba namba akasema nitakupigia tuongee, nikasema sawa.
Sikumtafuta wala hakunitafuta kama wiki mbili hivi. Sasa Siku hiyo ilikuwa ijumaa akanipigia simu kuniomba tuonane. Aliomba usiku akitoka kazini tukutane mahali kwa dinner, nikasema sawa. Sasa siku hiyo nilikuwa na ratiba ya kwenda kanisani ibada ya jioni, hivyo nikaenda kanisani kwenye Ibada nikatoka mida ya saa kumi na mbili na nusu jioni, akanipigia simu uko wapi nikamwambia niko kanisani ndio natoka, akastuka umetoka kanisani tena, nikamjibu ndio nilikuwa Ibadani. Akasema basi nitakutafuta wiki ijayo, nikamwambia ndio nilikuwa najiandaa kuja tuonane akasema hapana next week.
Nilipata mashaka lakini nikapotezea.
Hakunitafuta tena mpaka jumanne, akanipigia akaniuliza leo unaenda kanisani? Nikamwambia hapana. Akasema kama hautaenda basi tuonane jioni. Akaniambia nakuomba sana usiende kanisani, tuonane kwanza nikamwambia sawa. Sijakaa vizuri akanitumia Laki tano kwenye simu akasema huwa sitembei na Cash naomba wewe ndio ulipie gharama zote tutakazo tumia kwa dinner nimekutumia hela, na chagua twende wapi, nikasema sawa. Nikamwambia ninapotaka kwenda, akasema sawa basi tukapanga tukutane huko saa mbili.
Ni Mkaka ambaye anavaa macheni mengi makubwa, na mapete makubwa vidoleni, kiufupi ni Mtu anayejipenda. Nilifika pale hotel akaniambia nishafika nikamuona anashuka kwenye Prado nyeupe mpyaaa, na ana driver na Mtu mwingine kama mlinzi. Kiukweli nilisema moyoni kuwa nimeopoa Dodo kwenye mkorosho. Mimi kutongozwa na tajiri aisee ni bahati.
Basi tukafika tukakaa tunaongea, akaniambia Yeye hana Mke, Mke wake alishakufa, ila anawatoto wanasoma nje ya nchi. Akanionyesha Picha. Akasema Mimi nimekuona nimekupenda nataka uwe mpenzi wangu. Sisemi kwamba nitakuoa leo au kesho ila naomba uwe mpenzi wangu, unisaidie kupunguza stress huko mbeleni basi tutafunga ndoa. Huwezi amini niliitikia pale pale SAWA HAINA SHIDA 😂😂 sikuwa na sababu ya kukataa. Basi tukala tukaongea tukaondoka.
Nilifika nyumbani nikamwambia asante kwa dinner, akanijibu nashukuru Mke wangu na hapohapo akanitumia Million 1 kwenye simu akasema nataka jumapili hii tutoke tena. Naomba ukanunue nguo nzuri, kiatu uende na salon. Napenda mwanamke anaependeza na kunukia. Nikastuka nikasema sawa. Akasema katafute Wig zuri nataka uwe mwanamke wa kisasa. Kiufupi sikulala usiku namuwaza Yeye.
Sio siri nilichanganyikiwa na huyu mwanaume, jamani Jamani yani nilikuwa tayari kulala nae bila shida na nilikuwa tayari hata nihamie kwake hata kesho, kiufupi nilipagawa nae.
Cha ajabu sasa, nilienda nikatoa ile hela nikaenda shopping jamani nilirudi nyumbani sina hata senti, nikajiuliza nimenunua nini mbona vitu vichache hela imeisha? Nilijilaumu sana ila nikasema niache next time nitakuwa makini.
Sehemu Ya Pili ...✍️
KUMBUKA APPOINTMENT ILIKUWA NI JUMAPILI, hivyo nikandaa vitu jumamosi nikaenda salon nikajipodoa hatari ili jumapili nikitoka tu ibadani nijiandae nitoke.
Huyu mwanaume hakuwa mwanaume wa kuchat wala kupiga simu sana. Anaweza akatuma message moja ukamjibu, yeye hajibu tena mpaka jioni. Hivyo kwakuwa tulipanga tuonane jumapili saa 12 jioni basi nikasema nifanye mambo yangu jioni nimcheck.
Jumapili asubuhi kama kawaida nikaingia kanisani, siku hiyo nilipendeza sana na nilikuwa nafuraha sana jamani, yani kuna muda nilitamani nishike Mic nishuhudie kanisa kuwa nimepata mwanaume tajiri. Siku hiyo niko Ibadani lakini niko so excited natamani jioni ifike haraka nikamuone mpenzi wangu. Hivi ushawahi kuwa na furaha na kitu mpaka unasikia kusisimka mwili. Ndio Mimi sasa , yani najikuta tu niko excited 😂😂
Nikatoka Ibadani nikarudi nyumbani kujiandaa mida ya saa kumi kanipigia, Yes Mke wangu uko wapi, Mimi tena nikamwambia nimetoka kanisani niko nyumbani najiandaa kuja tuonane Babaa. Akastuka aaaah umeenda kanisani basi tutaonana wiki ijayo.
Nikamwambia kwanini hutaki kuonana na Mimi nikitoka kanisani, akasema wewe unajua taratibu za kanisa haifai kisali huku unazini. Mimi nakuomba achana na mambo ya kanisani Mke wangu, sisi tuenjoy tukitaka kuoana tutaenda. Nikamjibu sawa. Akasema basi wiki ijayo.
Nilijisikia vibaya moyo uliuma, nilikuwa nimemmiss sana jamani, nilitamani nimuone. Basi usiku nikawa chumbani nalia tu na sijui nalilia nini , kesho yake asubuhi nikampigia nikamwambia nimeshindwa kuvumilia naomba nikuone mpenzi nakuomba. Nisamehe sitaenda tena kanisani. Nililia nikaomba msamaha. Akanijibu sawa washa gari njoo sehemu fulani. Kazini nikampigia Boss kuwa ninajisikia vibaya naomba nije kesho. Nikajiandaa huyooo mpaka hiyo sehemu, ni nyumbani kwake Nilivyofika nilifurahi kumuona jamani sijui ni kitu gani ila nilimpenda ghafla, yani ghafla nilijikuta namuhitaji. Basi jumatatu ile nikajikuta nimefanya nae mapenzi, na hapo Ndio shida ilianza. Nikajikuta sitaki kuondoka nikamwambia nalala hapa hapa jamani, nikalala mpaka asubuhi akaniambia nenda kazini jioni tuonane. Nikarudi nyumbani nikavaa nikaenda kazini, nikabeba na nguo zangu nyingine nikasema leo sirudi nalala huko huko. Jamani nilikuwa kama nimepagawa, jioni nilijipeleka mwenyewe nikalala nae pale, kiufupi nilikaa pale wiki mbili na alinitumia kila siku.
Alikuwa ananipa pesa nyingi sana sana na nilifurahia hayo maisha.
Akaniambia kama unataka kuwa na Mimi sitaki marafiki, sitaki kanisani wala maombi, naomba utulie ndani nitakupa kila unachotaka. Hata kazi baadae utaacha tu. Nikajibu sawa, yani nilikuwa mjinga jamani.
Nilikaa kwake mwezi mzima, simu napigiwa sipokei, wazazi hawanipati, kanisani hawanioni, watu wananitafuta nawablock. Nilijikuta nachukia kila mtu mpaka ndugu zangu nampenda Mpenzi wangu tu.
Na alikuwa Mtu wa kununanuna na sio muongeaji, akikasirika ananuna HAONGEI, na Mimi sikuwa napenda hiyo hali hivyo muda wote nikawa najishusha. Niliishi maisha ya kifahari, nilikuwa na pesa na nilienjoy kwakweli, japo sasa nilijikuta nachukiwa na watu bila sababu. Kazini Boss akaanza kuwa mkali ananichukia na akasema atanifukuza kazi. Jambo dogo tu linakuwa kesi. Nikaanza kupoteza pesa, kila pesa ninayoipata inapotea, ofisini nikajikuta nimepata Loss kubwa sana mpaka nikaandikiwa barua ya kupumzika kwanza wafwatilie deni limekuwaje kubwa.
Baadae nikaanza kuumwa, yani najikuta mwili hauna nguvu, naishiwa nguvu hata kutembea siwezi. Hospital wakasema sina damu, ikabidi nilazwe niongezewe damu. Baadae nikadevelop tatizo lingine la tumbo. Nilikuwa nableed damu nyingi yenye mabonge mabonge na maumivu makali ya tumbo.
Akanipeleka hospital wakasema nina uvimbe na ili nipone natakiwa nitolewe kizazi. Mpenzi wangu hapo hapo akasema sawa kabisaaa toa tu kizazi. Nikashangaa natoaje kizazi ghafla hivi. Mbona nawajua watu wanauvimbe tumboni na wanatembea nao. Mimi hata sijazaa hapana. Nikamwambia sitoi kizazi acha nitulie kwanza.
Hali iliendelea kuwa mbaya sana sana, siku hiyo nilianza kubleed mfululizo, yani nableed damu haikatiki. Na chaajabu huyu Baba hana kinyaa ananiogesha, anafua nguo za damu na kuna siku damu ilimwagika chini kama li nyama akasema mbona kawaida akaliokota akalila. Niliogopa, akaniambia nakupenda sana mpenzi, hiyo damu yako kwangu ni chakula kabisa. Sio kwa ubaya ila huku na bleed alikuwa usiku ananinyonya huku chini anakunywa damu 😭😭.
Nikajiuliza huyu mwanaume nimemchanganya na kitu gani mpaka anywe damu yangu. Alinionyesha Upendo sana. Alinijali mnooo. Na siku zingine anaamka usiku ananiambia Mke wangu naomba unisaidie, ninakiu naomba ninywe damu, basi naenda naoga nakaa ananyonya damu hata nusu saa. Akimaliza ananishukuru mnooo mnoo hadi anapiga magoti na ananipa pesa sana.
Sasa huo ndio ukawa mchezo wake usiku ananyonya damu, na asubuhi kabla hajaoga ananiomba Mke wangu naomba ninywe damu ninakiu, basi ananyonya baadae anajiandaa kwenda kazini. Imagine hata akiwa kazini ananiambia nakupenda Mke wangu, nimemiss kunywa damu yako, ni tamu. Nikasema jamani Mimi naumwa lakini huyu Mtu ndio kwanza anaenjoy hizo damu. Yani damu ikikatika anakosa raha, anasema jamani natamani itoke ninywe. Siku ikianza atawahi kurudi nyumbani na usiku atakesha kunywa. ..
Follow me then turn on post notification uwe tayari kwa muendelezo 😃
Story kama hii usikubali ikupite wakati kila siku saa 2 usiku nakuletea hapa hapa
Hii account ni yenu muifollow ikuwe 🙏
@Kingvannytz_
Niko hapa nawaandikia muendelezo naomba msiniangushe mnifollow basi nizidi kuwaletea kazi nzuri 😊🙏
Gusa 👉 @Kingvannytz_ kisha follow me na kuweka notification on kwa post zangu 🙏
Mje mpate na dawa hapa 👇
x.com
Suluhisho la magonjwa mbalimbali liko Maasai Herbal Clinic
x.com

جاري تحميل الاقتراحات...