11 تغريدة 9 قراءة May 31, 2024
Vyakula 10 vinavyosaidia kuongeza nguvu za kiume kwa muda mfupi
1. Tangawizi
Zinajulikana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula
2. Asali
Baadhi ya vitamini vinavyopatikana kwenye asali ni pamoja na ascorbic acid, pantothenic acid, madini yanayopatikana kwenye asali ni pamoja na calcium, copper, iron, magnesium. Vitamini na madini hayo husaidia katika uzalishaji wa homoni ya testosterone na mbegu za kiume
3. Karanga
Inasaidia kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu katika mwili. Ongezeko la mzunguko wa damu kwenye uume humuwezesha mwanaume kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua
4. Chaza na Pweza
Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji chumvi. Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.
5. Parachichi
Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa testosterone, homoni ya kiume. Inatajwa kuwa wanaume wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali wa kimapenzi.
6. Ndizi mbivu
Zina kiwango kikubwa cha potasiamu ambacho husaidia kuongeza uzalishaji wa testosterone, homoni ya kiume na kuboresha hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume
Tryptophan iliyopo ndani ya ndizi mbivu husaidia kuongeza serotonin, homoni inayoboresha hisia na kuongeza hamu
7. Tende
Ni aphrodisiac ya asili, hivyo kula tende kunaweza kusaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume. Tende zina kiwango kikubwa cha madini ya chuma, vitamini c, folate nk.
8. Tikitimaji
Tikiti maji lina kiasi kikubwa cha asidi ya amino (L-citrulline) ambayo inachochea mtiririko wa damu kwenye uume. Wanaume wenye tatizo la uume kutosimama na hamu ya chini ya tendo la ndoa (low libido) wanaweza kunufaika kupitia L-citrulline kwa kula tikiti maji
9. Pilipili
Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo humuwezesha mwanaume kusisimka haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa.
10. Matunda na Mboga za Majani
Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta. Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.
Thank you for your time
Follow me and I will follow you back
@heisbixen
@heisbixen
@heisbixen
@heisbixen
@heisbixen
Goodbye 👋

جاري تحميل الاقتراحات...