Mfalme 👑🇹🇿
Mfalme 👑🇹🇿

@MfalmewaX

2 تغريدة 6 قراءة Apr 06, 2024
Unapokuwa mwanaume wa hisia hisia, inamaana ni rahisi kuumia, kupelekeshwa na chochote kilichopo mbele yako.
Hata hisia za kuangalia video za X au kujichua zinapokujia, zinakushinda na unajikuta unajiumiza zaidi.
Japo akilini unajua ni mbaya lakini hisia zina nguvu na zinakushinda.
Kwasababu upo laini laini kihisia.
Mwanaume inabidi uwe ngangari kihisia, usiruhusu hisia zikuendeshe bali akili.
Wanaume wengi wanaendeshwa sana na hisia, hisia inayomjia ndiyo hiyo hiyo anafanyia kazi. Kama vile mwanamke.
Hii inatokana na dunia ya sasa inayosema 'unaruhusiwa kuwa na hisia'
Dunia ya kike. Feminized world.
Inayochochea masculinity kufa.
Masculinity inaongozwa na akili, misimamo, heshima mipaka na malengo.
Masculinity ndiyo uanaume wako. Ndiyo dignity yako.
Haitaki uendeshwe na hisia, bali na akili ili uweze kuongoza familia na mwanamke kwa akili.
Hisia waachie wanawake.
Na sio kwamba umeshikiwa bunduki ukilazimishwa uwe na uendeshwe na hisia kama mwanamke
Ila ni malezi na mambo unayoangalia mtandaoni au kwenye muvi.
Kadri unavyojiruhusu kuendeshwa na hisia, ndivyo unajisikia heshima yako inashuka.
Jichunguze na utaligundua hilo.
Sababu hisia hisia ni kinyume cha masculinity.
Badala yake, jitoe kwenye hii fantasy ya kwamba 'mwanaume na wewe uwe na hisia'
Hizo hisia zitakupelekesha na kuishia kujichua, kuwa dhaifu, kuendeshwa na mwanamke, kuwa muoga, n.k.
Na uvae uanaume (masculinity). Kwa kutumia akili katika KILA jambo.
Ukitaka kutumia akili kirahisi, anza kwa kujiuliza kwanini/ why kwa kila jambo.
Halafu ufanye kitu kama why yake ina faida kwako, kwa familia yako, jamii na taifa lako.
Na hiyo why imfanye Mungu ajisikie proud kwamba amekuweka hai hadi leo.
Acha kukubali kuendeshwa na hisia.
Cc @InfiniteKiumeni

جاري تحميل الاقتراحات...