19 تغريدة 10 قراءة Sep 15, 2023
ACHA KUTAZAMA  PORN.
UZI🧵
Uraibu wa Kutazama video za ngono unaathiri maisha yako kitabia, kiakili, kihisia na hata kiroho pia. Mazoea ya kutazama video za ngono yanaweza kuathiri maisha yako kwa kiasi kikubwa pale yanapotoka katika hali ya mazoea na kuwa TABIA.
Kuna sababu mbalimbali zinazochochea URAIBU wa kutazama video za ngono..
Kwa vijana ukosefu wa elimu ya udhibiti wa hisia, ukosefu wa elimu ya udhibiti wa matamanio yao ya kimwili, Ushawishi wa marafiki wa baya, pamoja na matumizi ya mabaya ya mitandao ya kijamii wakati wa
umri wao wa balehe hadi ujana ni miongoni mwa sababu..Lakini pia, watu wazima walio na uraibu wa kutazama video za ngono huitumia kama njia isiyofaa ya kukabiliana na msongo wa mawazo maishani mwao,unaosababishwa na kutokuridhika au kutoridhishwa katika mahusiano yao,
migogoro ya mahusiano yao, kutokuwa katika mahusiano, Nakadhalika. Ili kuacha kutazama video za ngono, Jambo unalopaswa kulizingatia ni kwanini unapaswa KUACHA.Kujua sababu kwanini unapaswa kuacha ni mkakati muhimu unaokuongoza katika kushughulikia URAIBU wako ulionao wa kutazama
Mtu ambaye ni mraibu wa kutazama video za ngono wakati wowote na katika mazingira yoyote, hata ambayo hayafai, Huwa katika matamanio makubwa ya kutazama video za ngono.
Zifuatazo ni Baadhi ya ishara zinazoashiria URAIBU huu...
1..Unajiona kuwa haiwezekani kuacha kutazama video za ngono hata unapotaka kuacha..
2..Unajisikia hatia au aibu kubwa kuhusu muda na rasilimali unazotumia kutazama video za ngono..
3..Unapuuzia kazi na mahusiano yako ya kibinafsi ili kutumia muda huo kutazama video za ngono...
4..Unaona huridhishwi au kufurahia kufanya ngono, au tendo la ndoa bila kuhusisha utazamaji wa video za porn
5..Unahisi kuwa kutazama video za ngono kumeathiri ufanisi wako au Kazi zako za maisha ya kila siku ikiwemo utendaji wako wa tendo la ndoa...
......ZINGATIA .......
URAIBU wa kutazama video za ngono ukipuuzia, unaweza kuwa matokeo mabaya ya kitabia, kiakili, kihisia na hata kiroho pia. Ikiwa dalili zilizoorodheshwa hapo juu ndizo unazozipitia, basi ni wakati wako wa kushughulikia URAIBU wako.
Vifuatavyo ni Baadhi ya vidokezo vinavyoweza kukusaidia kushughulikia URAIBU wako....
1.. Elewa Kwanini Unaacha. Sababu za kuacha zinaweza kuwa, unaacha kwasababu za kidini, kiimani au maadili. Unaacha kwa sababu inasababisha ugomvi kati yako na mpenzi wako.
2..Kubali kwamba una tatizo, hivyo tafuta usaidizi. Watu wengi huficha URAIBU wao kwa kutokuongea Kwa hofu ya kuhukumiwa na watu au jamii Kwa ujumla. Lakini, habari njema ni kuwa hauko peke yako Tafuta usaidizi wa tatizo lako ikiwemo kuzungumza na kiongozi wako wa dini..
3.. Usijilaumu wala kujichukia. Kujaribu kuacha tabia au kupona kutoka kwenye uraibu wa kutazama video za ngono ni safari. Kwa bahati mbaya, katika safari hiyo, unaweza kujikuta ukirudi kwenye mazoea yako ya zamani. Jambo hili linapotokea, usipoteze muda wako Kwa kujilaumu.
4..Badilisha Kutazama video za ngono kuwa ni tabia ya Afya. Njia inayoaminika ya kujikwamua na tabia isiyofaa ni kuibadilisha na kuwa tabia nzuri inayofaa wakati wowote unapoanza kuhisi hamu ya kujiingiza katika tabia hiyo mbaya.
Kwa mfano, Kufanya mazoezi wakati ya viungo vya mwili unapohisi hamu kutazama ponografia video za ngono ni njia nzuri.
........ Jinsi ya kuvunja Tabia isiyofaa, Matibabu ya uraibu wa kutazama video za ngono ......
Ikiwa unafikiri una uraibu wa kutazama video za ngono, kujaribu tu kuacha kutazama ponografia ni jambo gumu sana . Kwa hivyo, jambo la kwanza la kufanya unapozingatia matibabu ya uraibu wa ponografia ni kuzungumza na mtaalamu wa Afya ya akili ( Mwanasaikolojia au Mshauri nasihi).
Mazungumzo yako na mtaalamu wa Afya ya akili kupitia tiba ya mazungumzo yatatambua ikiwa kweli una uraibu wa kutazama video za ngono na kupanga hatua za matibabu zinazofuata za kukabiliana na uraibu wako.....
TUZIDI KUJIFUNZA, TUSICHOKE KUJIFUNZA....
Unaweza Bookmarks hii Tweet huenda ukahitaji haya mawazo siku moja au kumsaidia mwenzako.
| Mwisho |
Nashkuru kwa kupitia uzi huu nadhani utakua umejifunza kitu.
Tafadhali nijulishe ikiwa kuna kitu maalum ungependa niandike. Usisahau kulike, Kuretweet , Kufollow @heisbixen na Kucomment.

جاري تحميل الاقتراحات...