6 تغريدة 15 قراءة Sep 14, 2023
𝗪𝗮𝗮𝗻𝗱𝗶𝘀𝗵𝗶 𝘄𝗮𝗽𝘆𝗮 𝘄𝗮 𝗺𝗶𝘀𝘄𝗮𝗱𝗮 𝘆𝗮 𝗳𝗶𝗹𝗮𝗺𝘂(𝘀𝗰𝗿𝗲𝗲𝗻𝗽𝗹𝗮𝘆𝘀) 𝗵𝗮𝘄𝗮𝗺𝗯𝗶𝘄𝗶 𝗵𝗮𝘆𝗮!
Ni ukweli ulio wazi wengi wanajiaminia,
Uhakika uko mkubwa kuwa wanaandika kitu kizuri.
Ukiwasoma kiundani utagundua wanachowaza,
wengi wanawaza namna ya
kupata pesa kupitia maandishi yao.
Ni sawa, hilo ni jambo jema!
Lakini kabla haujataka kujua wapi utaweza kuuza #script yako,
Je umeipa thamani kazi yako?
Najua wengi mnataka kujua gharama za kuuza script zenu na wapi mtauza,
Ukweki ni kwamba hakuna soko rasmi wa bei elekezi
juu ya hilo!
Sasa nini ufanye?
JIUZE!!
Ndiyo, manunuzi huja pale watu wanapopata uhitaji,
Je wewe umefanya watu wahitaji huduma yako?
Andika #scripts fupi kadhaa Kisha uzifanyie filamu fupi.
Ndiyo, filamu fupi.
Kusanya marafiki na watu wa karibu,
Tumia hata #smartphone kupata
video,
#Mics za simu siku hizi ni nyingi na bei poa,
Shoot filamu yako,
hata kama ya dakika moja!
Uandishi mzuri utaonekana hapo.
Kwanini ufanye hivyo?
Ni ngumu mtu kuanza kusoma script ambayo hana Kazi nayo,
Halafu eti aipende na atake kununua.
Lakini ni rahisi mtu kutazama
video hata ya dakika 5 au zaidi,
Iwapo tu inavutia na kusisimua.
Muhimu Fanya kwa wingi na kwa ubora uwezavyo!
Utaaminika, utauzika.
Kuhusu gharama za script iwapo mtu akipendezwa na uandishi wako,
Hilo linategemeana na ukubwa wa project yake,
Huo unaenda sambamba na ukubwa
wa bajeti yake.
Jifunze kuuliza maswali sana ili kusoma mazingira ya kazi yake,
Kumbuka hii ni BIASHARA!
Wewe Ndiyo una Kazi ya kuiweka sokoni.

جاري تحميل الاقتراحات...