Stone Cutter
Stone Cutter

@jamzsjason

13 تغريدة 3 قراءة Jul 13, 2023
SUMA JKT tujifunze toka SAMSUNG kuikomboa #Tanzania kiuchumi. (Thread)
Tunaposherehekea miaka 60 ya JKT tunajivunia umahili na uadilifu unaoendelea kuwepo katika Jeshi letu la Kujenga Taifa pamoja na ubunifu wao katika SUMA JKT.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari jinsi gani Tanzania inaweza kupata taasisi kama SAMSUNG kampuni moja iliyoweza kulikomboa lililokuwa Taifa masikini la Korea Kusini.
SAMSUNG na SUMA JKT wanafanana sana. Wote ni makampuni binafsi yenye mkono wa Taasisi za Kiserikali.
SUMA JKT ikiwa ni Jeshi la kujenga Taifa JKT Tanzania na SAMSUNG ikimilikiwa kwa 7.92% na Mfuko wa Huduma za Pensheni wa Korea.
Makampuni yaliyo chini ya JKT
Makampuni yaliyo chini ya SAMSUNG
SAMSUNG ni alama ya Ushindi kiuchumi kwa watu wa Korea Kusini. Wanaipenda na kuithamini. SUMA JKT tunaipenda na kuikubali watanzania lakini ni wakati sasa iende hatua moja mbele.
1. SUMA JKT ibaki kusimamiwa na JKT
2. (Branding) Tuondoe neno JKT ibaki SUMA
3. Iweke % fulani za umiliki kwa umma hata 10% wananchi wananunue Shares DSE jina liwe SUMA PLC
4. SUMA LOGO iwe kibiashara na sio Kijeshi.
5. Iwe Sera / Vision ya kitaifa kuipeleka SUMA mbele kitechnolojia, miundombinu na Fursa zaidi za Kazi kuwezesha kukuta mtaji wake. Leo tunasema DP World ina mtaji ni kwa sababu serikali yao imeamua kuipa support kama alama ya Taifa. National Brand.
Tuweke taasisi kama SIDO, VETA na Shule za Ufundi kama sehemu ya SUMA PLC.
Simu ya Kwanza toka Tanzania, Gari la Kisasa toka Tanzania, Mapinduzi ya Kiubunifu na Exports zinatakiwa zitoke SUMA PLC. Tutengeneze Toothpick zetu wenyewe (inawezekana)
Hili jengo refu zaidi duniani limejengwa na SAMSUNG ENGINEERING. Sisi tuwaze SUMA Engineering (Inawezekana)
MELI KUBWA Duniani zinatengenezwa na SAMSUNG. Sisi Tuwaze SUMA Heavy Industries (Inawezekana)
Vifaru vya Kijeshi na vifaa vya Kijeshi vinatengenezwa na Samsung AeroSpace Industries. Sisi tuwaze SUMA AEROSPACE Industry (Inawezekana)
Bado Samsung ina Shirika la Bima, Hospitali na vingine vingi. Wasingeweza fanya yote haya kama wasingekuwa na mkono wa serikali Yao. SUMA PLC inawezekana. Tunade-militarize Brand pekee umiliki unaendelea kuwa wa JKT 80% tutunze nidhamu na uadilifu. @SuluhuSamia @tonytogolani

جاري تحميل الاقتراحات...