15 تغريدة 412 قراءة Mar 13, 2023
FAIDA ZA KULA KIDOLE CHA MWANAMKE.(BAMIA.
UZI🧵
Nikiwa Kama Prof.Bixen nikaona sio mbaya ni wasogeze faida yake na matumizi yake pia Kidole Cha mwanamke.
1. Michirizi na utonvu unaopatikana katika Bamia, husaidia kusawazisha Kisukari kwa kuzuia kiwango cha Sukari inayotumika katika mwili kutoka kwenye utumbo mkubwa.
2. Bamia husaidia kulainisha Utumbo mkubwa (large intestines) kutokana na kazi yake ya kulainisha choo.
3. Utelezi wa bamia huchuja uchafu unaoingia katika Kolestorali (cholesterol) na asidi ya Nyongo unaoingia kutoka kwenye Ini ambao usipo dhibitiwa huenda ikasababisha matatizo ya ki-afya.
4. Bamia hutumika kwa kutibu vidonda vya Tumbo inasaidia kusawazisha Asidi.
Muhimu Magonjwa
5. Asidi ya Kujirudia rudia na Kufunga Choo
Tafuna vipande sita vya Bamia bila kutumia dawa nyigine kilasiku na Asidi ya Kujirudia rudia na kufunga choo kutakwisha, inashusha Sukari kutoka 135 hadi 98
6. Pumu
Bamia ina Vitamin C ambayo inawafana watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe ya Bamia iliyopikwa huwa na miligramu 13 ya vitamin C.
7. Kidonda Ndugu (Cancer)
Bamia husaidia kuweka Utumbo kuwa na hali nzuri hivyo kupunguza uwezakano wakuugua ugonjwa huu wa Kansa hasa kwenye utumbo mkubwa.
8. Mishipa midogo ya Damu
Kula Bamia kwa wingi kunasaidia kuimarisha Mishipa midogo ya Damu.
9. Cataracts
Nusu kikombe cha Bamia iliyopikwa inakua na kiwango cha 460 IU ya vitamin A.ambayo inapunguza uwezakano wa kupata ugonjwa wa mtoto wa jicho (cataracts).
10. Usongo (Depression) na Kukosa Nguvu
Bamia ni mboga bora zaidi kwa wale wanaojisikia dhaifu, Kuchoka na wanao athirika na Usongo (depression).
Iwapo mwanamke unasumbuliwa na tatizo la kukosa ute ute katika uke wako, tumia njia hii rahisi kabisa.
Chukua bamia.
Bamia ni lile litumikalo kupikia mboga hususani mlenda au hata kwenye mchuzi ili kupata utelezi.
Chukua bamia zako uzikatekate katika vipande vidogo vidogo kisha uviloweke katika maji safi kwa siku nzima.
Matumizi.
Tumia maji hayo kwa kunywa kila siku kwa muda wa siku 21.
Hakikisha unaloweka mapya kila siku ili kupata dawa bora na safi.
Dawa ya pili ni kwa wanawake wenye majimaji mengi kwenye uke kiasi kwamba inakuwa kero kwa baba nanii akija kufanya yake.
Matatizo ni kama jinsia. Aliyepewa hili amenyimwa hili.
Wakati unalalamika huna mwingine analalamika imezidi hivyo basi tusidharau tatizo la kila mmoja wetu.
Ili kutibu tatizo hili  chukua asali na mafuta ya zaituni. Changanya  na uanze kutumia kwa kunywa kijiko kimoja kila siku kutwa mara  mbili.
Pia uwe unapakaa asali huko ukeni na baada ya nusu saa utasafisha kwa maji safi. Fanya hivi kutwa mara mbili hadi utakapofikia hatua uipendayo.
Ukijua mjulishe na mwenzako bila chuki moyoni. Rt ili iwafikie watu wengi zaidi.
| Mwisho |
Nashkuru kwa kupitia uzi huu nadhani utakua umejifunza kitu.
Tafadhali nijulishe ikiwa kuna kitu maalum ungependa niandike. Usisahau kulike, Kuretweet , Kufollow @heisbixen na Kucomment.

جاري تحميل الاقتراحات...