𝗠𝘂𝗱𝗮 𝗔𝘂𝘁𝗼 𝗣𝗿o͙ 🚘🕺🏽
𝗠𝘂𝗱𝗮 𝗔𝘂𝘁𝗼 𝗣𝗿o͙ 🚘🕺🏽

@MudaAutoPro

10 تغريدة 1,706 قراءة May 16, 2022
Kwa Dereva ni muhimu sana kuijua Gari na Vifaa vyake kwa majina, kazi zake na hata muonekano wake..
Hii itamsaidia sana kutoumiza kichwa baada ya Gari kupata tatizo.
LEO TUVIGUSIE VIFAA MUHIMU VYA GARI UNAVYOPASWA KUVIJUA
👇🏾👇🏾
1. REJETA (RADIATOR)
Kazi ya chombo hiki ni kuhifadhi kimimika cha kupooza engine
2. OIL
Kazi ya oil ni kulainisha vyuma vinavyokutana kwenye Gari, Oil ni muhimu saana kwenye engine ukosefu wa oil unaweza kusababisha injini kufa au kusimama (knock)
3. MAFUTA YA BREKI (BRAKE FLUID)
Kazi ya mafuta ya breki ni kusaidia Gari liwe na breki pamoja na clutch. Ni muhimu kukagua na kuhakikisha mafuta ya brake yawepo kwenye kihifadhio chake.
4. BETRI ( BATTERY)
Kazi ya betry ni kuhifadhi umeme na kusambaza kwenye Gari.
5. IGNITION COIL
Kazi ya ignition coil ni kukuza umeme unaotoka kwenye betry na kuingiza kwenye distributor nayo inapeleka umeme kwenye plugs ukiwa umepoa, plugs ndio zinatoa moto kwenye engine.
9. DISTRIBUTORS
Kazi hiki kifaa ni kugawanya moto kwenye engine na kufanya Gari liwe na mlio mzuri na nguvu. Distributors ina waya tano ukichomoa waya moja Gari itakua inamiss
7. PLUGS
Kazi ya plug ni kuchoma petrol kwenye engine. Plug inapochoka inabidi ubadilishe ili kuepusha Gari kumiss.
8. FUEL PUMP
Kazi ya fuel pump ni kuvuta mafuta kutoka kwenye tank kuyapeleka kwenye carburettor
9. CARBURATOR
Hii hupokea mafuta kutoka kwenye fuel pump na kuyachanganya na hewa kwa kipimo maalum na kuyapeleka kwenye engine.
NB: Gari za sasa zinatumia injector ambazo ni automated badala ya carburettor
10. ALTERNATOR
Hiki huchaji betri na kusaidia betri kutopungua moto wakati wote Gari linapokua linatembea.
11. SELF START
Kazi ya self start ni kuwasha Gari wakati gari likiwa bovu na haliwezi kuwaka lenyewe. Ule wakati wa kusukumwa kwa gari na kushtuliwa.
12. GEAR BOX
Mchakato wote wa mwendo wa Gari hufanyika hapa. kubadirisha gia kua na kasi au kupunguza kasi ya Gari
13. DIFFERENTIAL
Kazi ya chombo hiki ni kugawa mwendo unaotoka kwenye engine na kuupeleka kwenye matairi.
14. CUT OUT
Hiki kifaa hufanya marekebisho ya umeme kutoka kwenye altarnator na kwa kipimo cha Volt 12 kiingiacho kwenye betry.
Najua hatotoka Bure hapo master Sasa unahitaji Kuagiza au kununua used Gar kwa kuzingatia bajet yako Nipigie niifanye iyo kazi kwa uaminifu 🤝👇🏾

جاري تحميل الاقتراحات...